Wilaya tatu Morogoro zanufaika na elimu ya msaada wa kisheria
4 October 2023, 12:12 am
wananchi wakifuatilia mafundisho kutoka kwa mwezeshaji wa Morogoro Paralegal Center – Picha Isidory
Kituo cha msaada wa kisheria Morogoro Paralegal Center(MPLC), katika ziara ya uhamasishaji (outreach) kimebaini changamoto za kisheria kwa wakazi wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga, ambao wanakabiliwa na migogoro ya ardhi, ndoa na mirathi
Na; Isidory Matandula
Wanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria Morogoro, wamebaini kuwa, wananchi wengi wanakabiliwa na changamoto za migogoro ya ardhi, mirathi na ndoa.
kulia ni mwanasheria Recho Siwiti kusho ni mwananchi akipata msaada wa kishria – picha – Isidory
Hayo yamebainishwa na Recho Siwiti, alipohojiwa na Redio Pambazuko, akiwa katika kijiji cha Mbuyuni, wilaya ya Ulanga, kutaka kujua changamoto walizoibua zaidi katika mikutano ya uhamasishaji kwa wananchi.
Sauti ya Mwanasheria Recho Siwiti
Nao wananchi waliofikiwa na elimu hiyo, Selina Muhogo na Salma Bilauli wakazi wa kijiji cha Mbuyuni wilaya ya Ulanga, wamekiri kunufaika na mikutano hiyo, katika masuala ya sheria ya ardhi na mirathi.
Sauti za wananchi
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mbuyuni, Musa Nyimbe amekipongeza kituo cha msaada wa Kisheria Morogoro kwa mpango huo wa kutoa elimu kwa kuzunguka kwenye vijiji, umesaidia jamii juu ya masuala ya sheria, hasa yanayohusu migogoro ya ardhi na Mirathi.
Sauti ya mwenyekiti Musa Nyimbe
Mikutano hiyo imefanyika katika wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga yenye lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi na kutambua haki zao, chini ya mradi wa POWER, unaofadhiliwa na shirika la The Aga Khan Foundation.