Jamii imetakiwa kutohusisha Majukwaa ya wanawake na Siasa
14 August 2023, 6:55 pm
Jamii ya Kata ya Usangule Wilayani Malinyi wametakiwa kutohusisha Majukwaa ya wanawake na mambo ya kisiasa kwani majukwaa hayo yapo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi
Na Katalina Liombechi
Wanawake wa Jukwaa la uwezeshwaji kiuchumi Kata ya Usangule Wilayani Malinyi wamesema Miongoni mwa Changamoto zinazowakabili ni pamoja Baadhi ya wana Jamii kuhusisha Shughuli za Jukwaa na Maswaala ya Kisiasa.
Akisoma Risala katika Hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa Hilo Mtendaji wa Kata ya Usangule Bi Hellen George amesema kuwa watu wamekuwa na Mawazo hasi ya kuwa Jukwaa hilo lipo kwa maslahi ya Chama Fulani hali ambayo inawapa ugumu katika Utekelezaji wa Majukumu ya Jukwaa.
Aidha amezitaja changamoto zingine kuwa ni Ukosefu wa Mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za Kifedha,Mtaji mdogo wa Jukwaa pamoja na ukosefu wa jezi za Mpira.
Nao Baadhi ya Wana Jukwaa hao akiwemo mwenyekiti Janeth Kamguna na Avelina Mwinami wamesema Uwepo wa Jukwaa hilo umewasaidia kuwaunganisha na Fursa mbalimbali za Kiuchumi,kufahamu namna ya kujitambua na kukumbushana mambo mbalimbali yahusuyo Afya Ndoa na Malezi.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo Diwani wa Kata ya Usangule Mh Fadhili Liguguda amesema Watu waondoe dhana ya kuhusisha Jukwaa na Mambo ya Chama kwani Maudhui yake ni maalumu kwa akina mama wote pasi kujali Itikadi za vyama,Dini,wala kabila la Mtu.
Hata hivyo akizungumzia Changamoto ya Mikopo Diwani huyo amesema Halmashauri imekuwa kitoa Mikopo ya Asilimia 4 Kwa Vikundi vya Wanawake wenye sifa lakini baadhi yao wamekuwa wagumu kufanya Marejesho.