DC Kilombero: Zingatia matumizi sahihi uhifadhi mazingira
7 June 2023, 10:09 am
“Nawaagiza wananchi wa kijiji cha Chiwachiwa pamoja na viongozi kutunza na kuhakikisha miti 500 iliyopandwa katika shule ya msingi Chiwachiwa inakua”. Mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya
Na; Katalina Liombechi
Imeelezwa kuwa katika kijiji cha Chiwachiwa halmashauri ya Mlimba bado kuna changamoto za utekelezaji wa shughuli za uhifadhi wa mazingira kutokana na kutozingatia matumizi bora ya ardhi na kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo yaliyohifadhiwa.
Hayo yamesemwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Basili Mwaka wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo wilayani Kilombero yamefanyika katika kijiji cha Chiwachiwa halmashauri ya Mlimba.
Sauti ya afisa mtendaji wa kijiji – bwana Basil Mwaka
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya amekemea shughuli zinazoharibu mazingira huku akitoa wito kwa jamii kuacha mara moja huku akieleza kuwa mto Kilombero unategemewa kupeleka asilimia 65 ya maji yake katika mradi mkubwa wa uzalishaji umeme Bwawa la Mwalimu Nyerere hivyo anayefanya uharibifu katika vyanzo vya maji anahujumu mradi huo.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho na kuwaagiza viongozi kutunza na kuhakikisha miti 500 iliyopandwa katika Shule ya Msingi Chiwachiwa inakuwa.
Sauti ya Dc wa Kilombero Danstan Kyobya
Meneja wa shirika linalojihusisha na uhifadhi wa wanyamapori Afrika AWF Clarence Msafiri amesema wao wanaamini kuwa mifumo ya Ikolojia na Bionuai ndio msingi wa afya na maendeleo ya jamii hivyo kuna kila sababu ya jamii kutambua na kuwa waangalifu na shughuli wanazozifanya ili kunusuru mifumo hiyo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Sauti ya Meneja wa AWF – C. Msafiri
Diwani wa kata hiyo Nestory Kyerula na baadhi ya wananchi akiwemo Asunta Gabriel na mwanafunzi Grace Samuel wameshukuru ujio wa mkuu wa wilaya pamoja na kuamua kufanya maadhimisho hayo katika kijiji chao huku wakiahidi kuitunza miti iliyopandwa na kuendeleza shughuli za uhifadhi kwa kushirikiana na wadau.
sauti ya diwani na wananchi wa kijiji cha Chiwachiwa