Wanaushirika Kilombero wapatiwa mafunzo
26 April 2023, 2:46 pm
wanachama wa ushirika wa uvuvi,usindikaji na masoko wakifuatilia mafunzo{Picha na Elias Maganga}
Vyama vingi vya ushirika vimekufa kutokana na kutokuwa na elimu ya ushirika na kutokuwa na siri, hivyo wanachama wametakiwa kuitumia elimu waliyoipata ili kuundeleza ushirika huo
Na Elias Maganga
Wanachama wa chama cha ushirka cha Uvuvi ,usindikaji na masoko Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro,wamepatiwa mafunzo ya dhana ya ushirika ,uongozi bora na uendeshaji wa chama cha ushirika
Mafunzo hayo yametolewa na Benk ya NMB kupitia mwezeshaji Thobias Mkamate ambaye ni Afisa Mafunzo wa Benki hiyo ,amesema kuwa lengo la kuwapatia mafunzo wanachama wa ushirika huo ni kuufanya kuwa imara,endelevu ili uweze kukopesheka kiurahisi
Afisa Mafunzo wa Benki ya NMB Thobias Mkamate akitoa mafunzo{Picha na Elias Maganga}
Akielezea misingi ya ushirika Bwana Mkamate amesema inazingatia maadili ambayo ni kujitegemea,uwajibikaji,demokrasia haki ,usawa na mshikamano.
Sauti ya Afisa Mafunzo wa Benki ya NMB Thobias Mkamate akielezea misingi ya Ushirika
Akishukuru kwa niaba ya wanachama wa chama cha ushirika uvuvi,usindikaji na masoko Kilombero ,mwenyekiti wa ushirika huo Bwana Abubakari Mashamba,amesema vyama vingi vya ushirika vimekufa kutokana na kutokuwa na elimu ya ushirika na kutokuwa na siri, hivyo amewaomba wanachama kuitumia elimu waliyoipata kuundeleza ushirika.
Hata hivyo Bwana Mashamba amewakaumbusha wanachama kulipa hisa na michango ya kila mwezi kama walivyokubaliana kwenye mkutano uliyopita,kwani wanatarajia kuanza kukopeshana kwa ayule asiyechanga wala kununua hisa hatokopesheka
Mwenyekiti wa ushirika Bwana Abubakary Mashamba{Picha na Elias Maganga}
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kupitia elimu waliyoipata watahakikisha wanaitumia ili ushirika huo usonge mbele kama malengo ya chama chao kinavyojieleza.
Mwanachama wa chama chama ushirika Bwana Waziri chikula {Picha na Elias Maganga}
Sauti za baadhi ya wanachama wa ushirika