Serikali yakamilisha tathmini kwa Walioezuliwa nyumba zao Ulanga
25 March 2023, 2:58 pm
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Minepa katika Vijiji vya Kivukoni,Mbuyuni na Minepa walipatwa na Maafa ya Nyumba zao kuezuliwa na upepo Mkali ulioambatana na mvua,Serikali Wilayani Ulanga tayari imekamilisha zoezi la tathmini na taarifa hiyo imeshatumwa Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa wakisubiri utekelezaji wake
Na Katalina Liombechi
Jumla ya Sh Milion 86 Laki 9 na Elfu 92 mia 6 ni Gharama iliyopatikana baada ya Tathmini iliyofanywa na wataalam katika nyumba za Watu Na Majengo ya Taasisi za Umma zilizoezuliwa na Upepo katika Kata ya Minepa Tarafa ya Lupiro Wilayani Ulanga.
Tathmini hiyo ni kwa Mujibu wa Maagizo yaliyotelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt Julius Ningu aliyoyatoa February 27 Mwaka huu baada ya kufika na kujionea namna nyumba za baadhi ya Wananchi wa Kata hiyo zilivyoathirika sambamba na kuzungumza na wahanga katika vijiji hivyo.
Kufuatia Maagizo hayo Pambazuko Fm imemtafuta Mkuu wa Wilaya huyo Dkt Ningu kutaka kujua majibu ya Tathmini hiyo ambapo amesema hesabu hiyo imejumuisha Majengo ya Taasisi za Umma ikiwa ni pamoja na Darasa moja katika shule ya Msingi Kivukoni ambayo gharama yake ni shilingi Milioni 20,Ofisi ya Walimu Katika Shule ya Msingi Kivukoni B laki 5 na Elfu 68 huku Kiasi kilichobakia ni Gharama ya Nyumba za watu
Gharama hizo ni kutokana na athali zilizojitokeza ambapo katika maafa hayo Vilivyoathilika ni Paa za nyumba ambazo baadhi ziliezekwa na nyasi na zingine kwa bati huku nyumba zingine zimeathiriwa mbao na tofari zilizotumika kujengea.Amesema Dkt Julius Ningu
Hata hivyo Dkt Ningu amesema Taarifa hiyo ameshaituma Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa ili kuona namna watakavyosaidia.
Hata hivyo Maafa hayo hayakusababisha Vifo isipokuwa Taasisi za Umma na baadhi ya Nyumba za watu kuharibiwa hali ambayo imewalazimu kujihifadhi kwa ndugu na majirani.
Ikumbukwe kuwa February 12 Mwaka huu Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Minepa katika Vijiji vya Kivukoni,Mbuyuni na Minepa walipatwa na Maafa ya Nyumba zao kuezuliwa na upepo Mkali ulioambatana na mvua hali iliyomsukuma Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt Julius Ningu kufika katika kata hiyo February 27 kujionea nyumba hizo sambamba na kuzungumza na wahanga ambapo alitoa maagizo ya Tahmini kufanyika kwa haraka ili kubaini athali zilizojitokeza.