Dc aagiza tathimini ya maafa kufanyika haraka
1 March 2023, 7:12 pm
Na Katalina Liombechi
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Dkt Julius Ningu amewaagiza wataalamu kufanya tathmini ya Nyumba zilizoezuliwa na upepo katika Kata ya Minepa ili Kupata takwimu sahihi za wahanga.
Mkuu wa Wilaya huyo ameyasema hayo February 27,Mwaka huu alipofika kujionea kaya hizo zilizopatwa na maafa kufuatia upepo Mkali ulioambatana na Mvua Mnamo February 12 Mwaka huu.
Baada ya kujionea nyumba hizo Mkuu wa Wilaya huyo amepata fursa ya kuzungumza na Wahanga hao ambapo amesema Timu ya Wataalamu watafika katika Kata hiyo kuchukua takwimu na baadaye atazipeleka katika Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa ili kuona namna ya kuwasaidia kwa kupunguza makali yaliyojitokeza.
Aidha amewapa pole kwa madhila yaliyowakuta na kuwaomba kuwa wavumilivu wakati wa mchakato huo huku akiwataka wawe tayari kupokea chochote kitakachotolewa na serikali.
Matumaini yao kusaidiwa na serikali na wadau wengine watakaoguswa
Wakizungumza Baadhi ya Wahanga wa Kijiji cha Mbuyuni Akiwemo Said Lyu,Zahara Kingumbi,Karim Masoud na Bakary Lupinga Wameshukuru ujio wa Mkuu wa Wilaya na Kuona namna walivyoathirika huku wakielezea maatumaini yao kusaidiwa na Serikali pamoja na wadau wengine watakaoguswa na hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kivukoni Shaneli Masasi amemshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo na kamati ya Ulinzi na usalama wakiambatana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ulanga kufika kuwaona wahanga sambamba na kuwapa pole hivyo amewataka kuwa wavumilivu hadi serilaki itakapowafuta machozi.