Chanjo ya kichaa cha Mbwa
22 February 2023, 3:31 pm
Isidory Matandula
Imeelezwa kuwa asilimia 99 ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa, wanakufa kwasababu waling’atwa na Mbwa mwenye kichaa na asilimia moja tu ndio wanakufa kwa kung’atwa wanyama wengine .
Hayo yamebainishwa na Dkt Sambo Maganga wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), Februari 18, mwaka huu, mjini Ifakara, katika mkutano wa viongozi wa jamii na wadau wa afya, kutoka maeneo yanayofanyiwa utafiti wilayani Malinyi mkoa wa Morogoro.
Dkt. Maganga amebainisha kuwa Mbwa huchanjwa kwa gharama kati ya shilingi 1,500 hadi shilingi elfu tano, na kwa upande wa binadamu amesema chanjo yake inapatikana kati ya shilingi elfu 30,000 hadi elfu 35,000 kwa dose moja, ambapo mtu mmoja anatakiwa kupata dozi moja hadi tatu ili kujikinga na kichaa cha Mbwa.
Utambuzi wa kiasi cha maambukizi ya kichaa cha mbwa na kutoa chanjo ni moja ya miradi mitano mipya inayotekelezwa na Idara ya EHES kwa sasa inayozingatia ikolojia na maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza .