Wazazi wamekubaliana kuchangia lishe shuleni
10 February 2023, 3:07 pm
Na Katalina Liombechi
Wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya msingi Ifakara katika Kata ya Viwanjasitini Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamekubaliana kuchangia lishe kwa watoto pindi wanapokuwa Shuleni ikiwa ni njia ya kukuza Ufaulu Shuleni hapo.
Katika Makubaliano hayo wazazi wamesema watachangia kila mzazi shilingi 1600 kwa Mtoto mmoja kutokana na kutambua umuhimu wa kufanya hivyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Esther Nuruva amesema watoto wanapokosa kupata lishe pindi wanapokuwa shuleni inapelekea kutokuwa na usikivu mzuri kwa mwalimu
Kwa Upande wake Mratibu Elimu kata ya Viwanjasitini Edwin Mkonga amesema kila mzazi anawajibu wa kuhakikisha mototo wake anapata lishe pamoja na huduma zingine muhimu kwani serikali inawajibika kwa Elimu Bure na mambo mengine.
Hata hivyo Mtendaji wa Mitaa ya Uwanja wa Taifa A,B,Viwandani Mhola na Viwanjasitini B,Ally Hassan Ally na Mwenyekiti wa Mtaa wa Uwanja wa Taifa A Charles Lyungu wamesema ni vyema wazizi wakatekeleza kwa hiyari waliyokubaliana kabla ya utekelezwaji wa Faini ya Shilingi elfu Hamsini.