Siku 16 za kupinga ukatili Ifakara
16 December 2020, 8:30 am
Kamati ya MTAKUWA kijiji cha Sagamaganga, kata ya Signali, kwa kipindi cha mwaka mmoja imefanikiwa kuibua ndoa na mimba za utotoni pamoja na matukio ya ubakaji.
Hayo yameelezwa na mjumbe wa kamati ya MTAKUWA wa kijiji hicho bi, MACRINA MHALAFU, katika mahojiano na Pambazuko fm, baada ya semina ya wadau wa kupambana na mimba na ndoa za utotoni iliyoandaliwa na shirika la WISE.
Bi MACRINA amesema kuw katika ita hivyo kamati yao imefanikiwa kuibua ndoa tatu za utotoni, mimba tatu za utotoni na tukio moja la ubakaji.
Kwa upande wake mwezeshaji wa shirika la WISE bwana EDMUND GAMA ameeleza mikakati kadhaa ya kuimarisha ufanisi wa kamati za MTAKUWA zinazoonekana kutofanya vema katika majukumu yake.
Lengo la semina hiyo ameeleza kuwa ni kubadilishana uzoefu na kuangalia baadhi ya changamoto zinazokabili kamati za MTAKUWA katika kupambana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
Insert: Gama – Malengo