Boma Hai FM
Boma Hai FM
19 March 2026, 11:02 pm

Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amefuturisha misikiti tisa katika jimbo la Hai akitoa ujumbe wa kudumisha umoja na mshikamano baina ya waumini wote wa dini zote.
Na Annasta Urio, Hai-Kilimanjaro
Wananchi na waumini wa dini ya kiislamu wilayani hai Mkoani Kilimanjaro wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la hai Saashisha Elininkio Mafuwe kwa kuwaunganisha kupitia futari .
Hayo yamejiri katika msikiti wa Nuru (matopeni ) march 18,2026 ambapo wananchi mbalimbali kutoka misikiti Tisa (9) iliyopo kata ya Bomang’ombe wamekutana pamoja kwaajili yakushiriki katika ifutari iliyoandaliwa na mbunge huyo.
Katibu mwenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai Mohamed Msalu ambaye amezungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM wilaya amemshukuru Mbunge Saashisha Mafuwe kwa kuelendelea kuwa karibu na wananchi wake bila kujali itikadi za kidini huku akieleza kuwa katika futari hiyo wameshiriki watu wa dini tofauti kuonesha ushirikiano na mshikamano wa wananchi wa wilaya hiyo.
Nae,Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya hai Omary Maamoud ambaye ndiye ostazi wa msikiti wa Nuru ameeleza furaha yake kwa kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge nakutoa shukrani zake kwa niaba ya waislamu wote wa kata ya Bomang’ombe kwa kuwakutanisha pamoja na kusema kuwa Dua zao zipo pamoja nae

Nae,Diwani wa kata ya Bomang’ombe Evod Njau ameshiriki katika zoezi Hilo la kufuturisha ambapo amempongeza Mbunge wa Jimbo Hilo kwa kuwaleta pamoja wananchi wake katika kuhakikisha anatengeza jamii yenye usawa na Umoja.
Kwa upande wake Neema Munisi ambaye ni muhumini katika msikiti wa Nuru amesema kuwa zoezi Hilo la kufuturisha limeenda vizuri kwani watu wamekula na kunywa hivyo wanamashukuru na kumpongeza Ndug.Saashisha na kuomba aendelee kushirikiana na jamii ili kutatua changamoto mbalimbali.