Boma Hai FM
Boma Hai FM
4 March 2026, 1:39 pm

Wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayotarajiwa kufanyika machi 9 2026 katika viwanja vya shule ya sekondari Mailisita.
Na Salma Mgosso
Hai-Kilimanjaro
Mratibu wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani wilaya ya Hai Catherine Peter, amewakaribisha wananchi wa makundi yote kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro kushiriki katika maadhimisho ya kimkoa yatakayofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Mailisita kata ya Mnadani.
Amesema wilaya ya Hai imejipanga kuhakikisha maandalizi yanakamilika kwa wakati na kwamba mazingira ya tukio yatakuwa salama na rafiki kwa washiriki wote, wakiwemo wanawake, wanaume na vijana.
Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yatatoa fursa ya kujadili haki na usawa wa kijinsia, pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hata hivyo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuonyesha mshikamano na kuunga mkono jitihada za kuimarisha nafasi ya mwanamke katika jamii, akisisitiza kuwa ushiriki wa kila mmoja ni muhimu kwa mafanikio ya tukio hilo.