Boma Hai FM
Boma Hai FM
27 January 2026, 4:43 pm

Machame Magharibi wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupanda miti pembezoni mwa Barabara kata ya Machame Magharibi
Na Vivian Kweka, Hai-Kilimanjaro
Diwani wa kata ya Machame Magharibi Martin Munisi amewataka wananchi kuacha kukata miti hovyo na badala yake wafuate vibali vinavyotolewa na mamlaka husika kwani kumekua na tabia ya baadhi ya wananchi kukata miti hovyo na kusababisha uharibifu wa mazingira.
Ameyasema hayo Januari 27 ,2026 wakati akiongoza wananchi kupanda miti mia tano kwenye eneo la hifadhi ya barabara katika kuadhimisha siku kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba wananchi wameshiriki kikamilifu katika shughuli hiyo, wakionyesha mshikamano wa kijamii.

Aidha,Diwani Munisi pamoja na wananchi wa kata ya Machame Magharibi wamemtakia maisha marefu na afya njema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kwamba wanaungana na watanzania wengine katika siku hii muhimu kwa Rais Dkt Samia.
Hata hivyo Kata ya Machame Magharibi inaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika uhifadhi wa mazingira na shughuli hii ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha kuwa mazingira yanahifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.