Boma Hai FM
Boma Hai FM
22 January 2026, 6:26 pm

Bodi ya Maji Uroki Bomang’ombe wametumia fedha za mapato yao ya ndani ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa wilaya ya Hai, mkuu wa wilaya ya Hai na Viongozi wengine wamepongeza juhudi hizo za kutatua adha ya maji kwa wananchi.
Na Gasper Joseph, Hai-Kilimanjaro
Mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko ameipongeza bodi ya maji Uroki Bomangombe kwa jitihada zake za kupunguza kero ya maji kwa wananchi kwa kutumia fedha za mapato yake ya ndani.
Bomboko ameyasema hayo wakati wa kupokea mabomba ya kupanua mradi wa maji Uroki Boma ngo`mbe yenye thamani ya shilingi milioni 120 kwa ajili ya ya mradi mpya wa chanzo cha mkomoshini unaolenga kuongeza maji takribani lita laki nane kwa siku.
Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai ambae pia ni diwani wa kata ya Muungano Muh Edimundi Rutaraka ameishukuru bodi ya maji Uroki Bomang`ombe Pamoja na RUWASA kuona umuhimu wa kutumia vyanzo vyake vya ndani na usimamizi mzuri wa rasilimali zilizopo kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye mrdi huo utakao ongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Hai Wang`uba Maganda amesema kuwa ilani ya chama hicho imetendewa haiki na bodi ya maji Uroki Bomang`ombe kwani maji ni huduma muhimu kwa jamii na chama chake kinasimamia huduma ziwe bora kwa wananchi.

Akizungumza wakati akitambulisha mradi huo meneja wa maji bodi ya maji Uroki Bomang`ombe mhandisi Arnold Mbaruku amesema kuwa bodi hiyo inatekeleza mradi huo kwa makusanyo yake ya ndani kwa zaidi ya shilingi milioni mia mbili hadi kukamilika kwake ili kuongeza na kuboresha huduma yam aji kwa wateja wake.