Boma Hai FM
Boma Hai FM
1 December 2025, 3:30 pm

Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt Christopher Timbuka, amewataka watumishi wa Halmashauri kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji mpya Hellen Mwembeta, ili kufanikisha jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.
Na Bahati Chume Siha-Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Siha, Christopher Timbuka, amewataka watumishi wa Halmashauri kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji mpya, Hellen Mwembeta, ili kufanikisha jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.
Kauli hiyo imetolewa Novemba 29, 2025, kwenye ukumbi wa RC Sanya Juu, wakati wa kumuaga Mkurugenzi Mtendaji wa zamani, Haji Mnasi, na kumkaribisha Mkurugenzi mpya.
Timbuka amesisitiza kuwa maendeleo hufanikishwa kwa ushikiano, na matokeo makubwa hayawezi kupatikana na mtu mmoja tu. “Ushikiano imara wa watumishi uchochea mafanikio na utachoa maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla,” amesema.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji mpya, Hellen Mwembeta, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa nafasi hiyo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii, akiwataka watumishi wote kushirikiana ili kufanikisha malengo ya wilaya.
Mkuu huyo wa wilaya pia amempongeza Mkurugenzi wa zamani, Haji Mnasi, kwa kazi nzuri aliyoacha, akisema matunda yake yanaonekana na yatabaki kuwa fundisho kwa wengine.
