Boma Hai FM

Rutaraka aibuka mshindi kugombea uenyekiti Hai

1 December 2025, 2:58 pm

Pichani ni aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka na ambae ameshinda katika uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi wilaya ya Hai kugombea tena nafasi hiyo(picha kutoka maktaba)

Edmund Rutaraka amethibitisha nguvu zake wilayani Hai baada ya kushinda kwa kishindo uchaguzi wa ndani wa CCM, akipata kura 15 kati ya 23 na kurejeshwa rasmi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai.

Na Elizabeth Mafie na James Gasindi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Edmund Rutaraka ameibuka mshindi katika uchaguzi wa ndani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Hai na kurejeshwa kugombea nafasi hiyo.

Rutaraka amepata kura 15 kati ya kura 23 zilizopigwa, akiwashinda madiwani Emmanuel Mgonja aliyepata kura 7, na Evod Njau aliyepata kura 1.

Katika uchaguzi huo huo, madiwani wamempitisha Trael Mboya kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri  ya wilaya ya Hai baada ya kupata kura 21 za ndiyo, huku kura 1 ikiwa ya hapana na 1 ikiharibika, akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.

Matokeo  hayo yametangazwa leo Disemba 1, 2025 na katibu wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Hai Mkaruka Kura.

Sauti ya katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Hai Mkaruka Kura.