Boma Hai FM
Boma Hai FM
17 October 2025, 10:57 pm

waendesha Bajaji wilaya ya Hai wametakiwa Kuzingatia Sheria za Barabarani na taratibu za usafirishaji ili waweze kufanya shughuli zao kwa weledi ndani na nje ya wilaya ya Hai,pia wameaswa kuwa mabalozi wa amani na usalama katika wilaya ya Hai.
Na Henry Keto, Hai- Kilimanjaro
Waendesha Bajaji wilaya ya Hai wametakiwa kuzingatia Sheria za barabarani pamoja na usafirishaji kwa kubeba abiria kulingana na ukubwa wa chombo chao na kufanya kazi kwa weledi ndani na nje ya wilaya ya Hai
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe.Hassan Bomboko alipokuwa akizungumza na Waendesha Bajaji katika mkutano Mkuu wa Waendesha Bajaj uliojumuisha Waendesha Bajaji zaidi ya 650 wanafanya shughuli za usafirishaji wilaya ya Hai.
Pia amewataka Waendesha Bajaj kuwa mabalozi wa ulinzi na usalama kwa kufichua wahalifu wanaowabeba au kuwaona, pia amewaonya wao wenyewe wasiwe wasafirishaji wa madawa ya kulevya bali wawe watu safi watakaoshirikiana na jeshi la polisi kulinda amani katika mji wa Bomang’ombe.

Bomboko ametoa maagizo kwa viongozi wa mamlaka ya mji mdogo wa bomang’ombe pamoja na afisa biashara kuwasajili waendesha Bajaji kama Machinga na wawekwe kwenye kundi la wajasiriamali wadogowadogo, vilevile emewataka kutoa elimu kuhusu kuegesha vyombo vya moto kabla yakuwakamata, baada yakutoa elimu wasajili maeneo yote ya maegesho yatambulike ndio shughuli za ukamataji wa wanaogesha vibaya na maeneo yasiyo sahihi.
Nae Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Hai OCD Oscar Joshua Ngumbulu amewataka Waendesha Bajaji wote kutumia vyombo vyao kwa kuzingatia Sheria na miongozo iliyowekwa na serikali, vile vile ametoa wito Kwa wasafirishaji kuwa na leseni hai ya kufanya shughuli zao, pia ametoa wito Kwa wasafirishaji kujitokeza kupiga kura bila shaka kwani ulinzi na usalama upo wakutosha.

Mkutano huo Mkuu wa Waendesha Bajaji amehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Afisa maendeleo ya jamii, Mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Bomang’ombe, jeshi la ulinzi na usalama wilaya ya Hai, pamoja na Waendesha Bajaji zaidi ya 650 waliosajiliwa.