Boma Hai FM

Hai waombwa kujitokeza kumpokea Dkt. Nchimbi

11 September 2025, 6:05 pm

Pichani ni Katibu wa siasa uenezi na mafunzo wa ccm wilaya ya Hai ndugu Mohamed Msalu (Picha na Henry Keto)

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuhutubia wananchi wa Hai, Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Wilaya ya Hai Muhamed Msalu ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi.

Na Elizabeth Noel & Henry keto, Hai-Kilimanjaro

Wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wameombwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo wa CCM wilaya ya Hai Ndugu Mohamed Msalu ameyasema hayo leo Septemba 11, 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Hai.

Sauti ya Katibu wa Siasa,uenezi na mafunzo wilaya ya Hai Ndugu Mohamed Msalu akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ujio wa mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya Ccm Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.

Dkt. Nchimbi anatarajiwa kuwasili wilayani Hai siku ya Jumamosi Septemba 13,2025 akitokea mkoani Arusha, na atahutubia wananchi katika viwanja vya Snow View, Bomang’ombe.

Msalu amesema maandalizi ya mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia kubwa, na amewataka viongozi wa chama, wanachama pamoja na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea mwenza akinadi sera za CCM.

Itakumbukwa kuwa kampeni za chama cha mapinduzi (CCM) zilizinduliwa rasmi Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Peckers vilivyoko Kawe jijini Dar es Salaam.