Boma Hai FM
Boma Hai FM
20 August 2025, 10:52 am

Kampuni ya APKL (African Partnership kilimanjaro Limited) inayojihusisha na shughuli za kilimo cha Kahawa Mkoani kilimanjaro zimefikia makubaliano ya kutia saini Mkataba wa Shamba la Ushirika la FONRWA lenye ukubwa wa hekari 205 uliofanyika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro
Na Henry Keto, Hai Kilimanjaro
Wawekezaji wilaya ya Hai wametakiwa kulinda rasimali zilizopo katika maeneo wanayowekeza pamoja na kutunza mazingira kwa Kupanda miti yakutosha ili kuendelea kulinda uoto wa asili na hali ya hewa .
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wilaya ya Hai Ndugu Sospeter Magonera wakati akishuhudia utiaji saini kati ya mwekezaji ambaye ni APKL na chama cha ushirikia cha FONRWA uliofanyika katika shamba hilo lililopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Pia amewataka wawekezaji kuendeleza kuyatunza mashamba hayo ambayo ni zawadi kutoka kwa mungu huku akiwasisitiza kuwa ardhi hiyo iliyotolewa na Mungu isiwagombanishe watu kwa dhuluma na wivu Kwa namna yoyote.
Sauti ya Katibu Tawala wa wilaya ya Hai ndugu Sospeter Magonera akizungumza wakati wa utiaji saini kwenye shamba la ushirika la FONRWA na kampuni ya APKL

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya APKL ( African Partnership Kilimanjaro Limited) Ndugu Anold Temba ameishukuru serikali na chama cha ushirika kwa makubaliano ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya mkataba wa shamba hilo lenye Hekari 205 ambazo kati ya hizo 25 zitakuwa ni Shamba Darasa kwaajili ya mafunzo Kwa wanashirika na Wananchi wengine, na nyingine ni kwaajili ya Kilimo cha Kahawa aina ya Arabica
Vilevile amesema kwa kipindi cha miaka kumi wamekuwa wakitoa ajira zaidi ya 940 kila siku na uzalishaji ukiendelea kukua Hadi kufikia gunia zaidi ya elfu 3000 kwa mwaka, amewasihi Wananchi kujitokeza kufanya kazi katika mashamba ya Kampuni ya APKL bila sababu pia kutoa ushirikiano kwa Wananchi na Kampuni katika mambo mbalimbali ya kijamii kama misaada na shughuli za kijamii.

Nae Mrajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika Bi Jacline Senzigwa Mkoa wa kilimanjaro Ameeleza vipengele mbalimbali kwenye mkataba na kuwaka wanashirika kuchangia pato la taifa na kuwaeleza wawekezaji kuwa wanatakiwa kutenga asilimia 10 kwaajili ya miradi ya jamii jambo ambalo ni takwa na vyama na mkataba kwa lengo la kurudisha kwa jamii na kulinda rasimali kwa jamiii.
Sauti ya Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kilimanjaro akizungumza wakati wa zoezi la utiaji saini wa mkataba kati ya FONRWA na APKL
Elisi simbo Muro ni Mwanaushirika wa FONRWA ambaye ameshiriku kwenye makubaliano ya utiaji sign kati ya chama cha ushirikia cha FONRWA na Kampuni ya APKL inayojihusisha na ulimaji wa zao la Kahawa kwa asilimia kubwa na mazao mengine kwa asilimia Chache, ameiomba Kampuni ya APKL kuzingatia mkataba waliosaini ili kuliendeleza shamba hilo ambalo limetekekezwa baada ya mwekezaji aliyekuwepo kumaliza muda wake mwaka 2O24 na kutoa kwa mwekezaji mwingine kwa muda wa Miaka 24 kuanzia mwaka 2025.
Sauti ya mshirika wa FONRWA akizungumza baada ya kushuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa shamba la FONRWA na kampuni ya APKL

Zoezi la makabuliano na utiaji Saini katika shamba la Ushirikia wa FONRWA na Kampuni ya APKL limeshuhudiwa na karibu Tawala wa wilaya ya Ha Ndugu Sospeter Magonera, ambapo mkataba huu ni WA MIAKA 25, na kila baada ya miaka 5 kapuni na chama cha ushirika watakutana kwaajili ya mapitio ya baadhi ya vipengele kwenye mkataba, uwekezaji huo unagharimu Zaidi ya Billioni 1.6