Boma Hai FM

Tanzania, Kenya kushirikiana utunzaji vyanzo vya maji

24 July 2025, 3:35 pm

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Raymond Mwagwala akizungumza na wadau mbalimbali wa maji (Picha na Elizabeth Noel)

“Lengo la msingi ndugu zetu wa Kenya na Tanzania  wameweza kuangalia ni wapi maji yanakotoka, wapi yanatakiwa yasafiri na watumiaji ni wapi. Safari hii itakuwa ya siku tatu na katika siku hizo watu watakuwa na nafasi ya kujifunza, kuangalia vyanzo vimetunzwaje lakini baada ya siku tatu kila mmoja aliyetembea katika safari hii aje na ushauri, awe amejifunza na tutatoka na maazimio ya pamoja.” Amesema Mwagwala

Na Elizabeth Noel Rombo- Kilimanjaro

Wadau mbalimbali wameanzisha safari ya maji iliyohusisha taifa la Tanzania na taifa la Kenya, yenye lengo la kuangalia vyanzo vya maji, kujifunza na hatimaye kuja na maazimio ya pamoja yatakayosaidia kufahamu namna ya kuendeleza na kuboresha vyanzo hivyo ili viwe na manufaa kwa mataifa yote mawili.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Raymond Mwangwala akizungumza katika uzinduzi wa safari hiyo uliofanyika katika kidakio cha maji cha mto Kimengelia kilichopo kwenye shamba la miti la North Kilimanjaro Rongai, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro amesema kuwa lengo ni kujenga mazingira ya uelewa na kuleta chachu kwa wananchi ili waweze kutunza na kubeba uhalisia wa uhusika wao katika utunzaji wa vyanzo vya maji.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mwangwala

Naye Jackob Sampeke, katibu wa masuala ya maji kutoka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ameshauri wataalamu kupanda miti rafiki inayosaidia kuhifadhi maji katika maeneo ya vyanzo vya maji.

Sauti ya Katibu wa Maji kutoka Kenya Jackob Sampeke

Kwa upande wake, Novat Kessy ambaye ni Meneja wa Miradi kutoka Shirika la WWF, ameeleza umuhimu wa kuwaunganisha wadau wa maji ili kusaidia serikali katika kulinda vyanzo hivyo.

Joel Naasi mhifadhi wa shamba la miti la Rongai, amesema kuwa shamba hilo lina mchango mkubwa katika kutunza vyanzo vya maji kupitia uhifadhi wa mazingira ya asili.

Sauti ya Mhifadhi wa shamba la miti Rongai Joel Naasi.