Boma Hai FM
Boma Hai FM
24 July 2025, 3:46 pm

Wanawake wanne wajawazito wamepatiwa msaada wa matibabu pamoja na zawadi baada ya kujifungua kutokana na ahadi iliyotolewa na mkuu wa polisi jamii wilaya ya Hai ASP Elishafra S. K wakati wa sherehe za jeshi la polisi wilaya ya Hai
Na Henry Keto, Hai-Kilimanjaro
Wanawake wanne wa Wilaya ya Hai wamepatiwa msaada wa matibabu kabla na baada ya kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Hai baada ya ahadi iliyotolewa na Mkuu wa polisi jamii wilaya ya Hai ASP Elishafra S.K baada ya kuwaalika wanawake hao kuungana na polisi kwenye sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa polisi wilaya ya Hai walipokuwa wanapita karibu na ukumbi huo July 15,2025
Mkuu wa Polisi jamii Wilaya ya Hai ASP Elishafra S.K ametimiza ahadi aliyo ahidi kwa wanawake wanne walikuwa wajawazito kuwasaidia kabla na mara baada ya kujifungua kwa kuwapa zawadi na kuwalipia gharama za huduma za hospital kama zitakuwepo.
Siku ya July 23,2025 Saa tisa alasiri ametimiza ahadi yake Kwa kuwatembelea wanawakehao wodini katika hospital ya wilaya ya Hai ambapo watatu kati ya wanne wamejifungua na ametoa zawadi za nguo za watoto na mahitaji mengine muhimu ya mama na mtoto.
Pia ametoa shukrani kwa mkuu wa kituo cha polisi na jeshi la police Tanzania kwa mafunzo ya polisi jamii, na kutoa wito kwa police wengine Kujitoa kuwasaidia watu wenye uhitaji na kuwaweka karibu ili kuwahudumia, amesema polisi sio watu wabaya hivyo Wananchi wasiwaogope wanapohitaji msaada kutoka kwao.
Sauti ya mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Hai ASP Elishafra S.K akizungumza baada yakuwatembelea wanawake wanne hosptali ya wilaya ya Hai

ASP Elishafra alitoa ahadi hiyo July 15,2025 wakati wa sherehe ya kuwaaga batch ya tatu na kuingiza batch ya nne katika ukumbi wa police mercy Wilaya ya Hai, ambapo wanawake hao walipita nje ya ukumbi huo wakaitwa kushiriki kwenye sherehe hiyo.