Boma Hai FM
Boma Hai FM
28 May 2025, 10:07 pm

Mafunzo ya udhibiti ubora wa mbegu za kilimo yanayotolewa na taasisi ya (TOSCI) kwenye mradi wa Youth Enterprenuership for the future of food and agriculture (YEFA)
Na Henry keto, Hai-kilimanjaro
Kaimu mkurugenzi wilaya ya Hai ambaye pia ni Afisa Kilimo wilaya David Lekey amewaasa vijana kuchangamkia fursa kwenye Kilimo hasa cha umwagiliaji.
Lekey amewaasa vijana wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwaajili ya elimu ya Udhibiti ubora wa mbegu za maharage lishe, yaliyoandaliwa na shirika la Youth Entrepreneurship for the future of food and agriculture (YEFA).

Afisa lishe mkoa wa Kilimanjaro Rehema Napegwa ameeleza umuhimu WA lishe hasa kwa akina mama na watoto, amesema mkoa wa Kilimanjaro una asilimia 20 sawa na watoto 48,000 wanahali ya udumavu jambo linalosababishwa na lishe duni.
Amewaasa jamii kuzingatia makundi yote sita ya vyakula ikiwemo jamii ya maharage lishe, ili kutenganisha kati ya nyama na maharage lazima tutumie vyakula mchanganyiko kwasababu maharage yana protein kama nyama lakn nyama ina mafuta mengi ganayosababisha uzito uliopitiliza
Afisa lishe wilaya ya Hai silvania kulaya amesema lishe ni muhimu hasa kwa wanawake wajawazito na wanaoenda kujifungua.
Amezungumza hayo wakati wa mafunzo ya Udhibiti ubora wa mbegu za maharage lishe anayotolewa na shirika la youth Entrepreneurship for the future of food and agriculture (YEFA) wakishirikiana na Taasisi ya kiserikali ya Tanzania Official seed certification institution (TOSCI)
Nae Marium mwambati ambaye ndie manager mradi wa YEFA amesema mradi huu utakuwa na tija kwenye Kilimo kwasababu katika jamii yetu kimekuwa na shida ya mbegu Bora, kwahiyo elimu hii itasaidia vijana kuwa wakulima waziri katika uzalishaji wa maharage lishe ili kuzalisha na kuongeza kipato na kufanya Kilimo chenye tija.

Nao vijana waliohudhuria mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika Kilimo chao ili kuongeza uzalishaji wa maharage