Boma Hai FM
Boma Hai FM
24 May 2025, 5:22 pm

” Kama mnavyofahamu wilaya hii ipo kwenye wilaya kumi za majaribio katika utoaji mikopo,niwajibu wetu kufanya vizuri ili na wengine wa wilaya zingine waweze kuiga “
Na Elizabeth Mafie -Siha Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Dkt Christopher Timbuka amevitaka vikundi vya wanawake,vijana na walemavu vilivyopata mkopo wa asilimia kumi ya halmashauri,kutumia mikopo hiyo kwa malengo walioainisha wakati walipokuwa wakiomba mikopo hiyo.
Kauli hiyo ameitoa Mei 23,2025 wakati akikabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya sh,300 milion kwa vikundi 46 katika ukumbi wa halmshauri ya wilaya ya Siha.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mfano huo wa hundi ,amevitaka vikundi vilivyopata fedha hizo,kwenda kutumia fedha hizo kwa malengo makhususi.
” Kama mnavyofahamu wilaya hii ipo kwenye Wilaya za 10 za majaribio katika utoaji mikopo,,niwajibu wetu kufanya vizuri ili na wengine wa wilaya zingine waweze kuiga “amesema Timbuka
Kwa upande wake Dancani Urasa Mwenyekiti wa halmshauri hiyo,amempongeza Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani na kwamba mikopo iliyotolewa kwa vikundi hivyo inatokana na makusanyo ya ndani ya halmashauri.
Nae mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Haji Mnasi amesema anamshukuru Rais Dkt Samia Suluhuu Hassani, kwa kurejesha utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa wananchi .
“Leo tumefanikiwa kutoa kiasi cha sh 300 milioni kwa vikundi hivyo vilivyotajwa baada ya wiki mbili zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi vingine kiasi cha Zaidi ya shilingi milioni mia mia tatu .Amesema Mnasi”

Samwel Adu afisa mtendaji mkuu wa bank ya uchumi wilaya ya Siha amesema kwa kushirikiana na halmashauri,wametoa elimu ya fedha kwa wanufaika wa vikundi 46 katika awamu hiyo ya kwanza.
Kaale lukundo mmoja ya wanufaika wa mikopo hiyo, amesema wanaishukuru halmshauri kwa mikopo hiyo na kuahidi kurejesha kwa wakati ili na vikundi vingine vinufaike.