Boma Hai FM

Bomang’ombe wamtwisha zigo la mbwa DC Bomboko

21 May 2025, 12:50 pm

Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wa kata ya Bomang’ombe katika mkutano wa hadhara (Picha na Eliya Sabai)

Katika kuhakikisha kila Mtanzania anaishi maisha bora na kupata huduma zote za kijamii, Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko amefanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi.

Na Eliya Sabai –Hai Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya Hai Mh Hassan Bomboko amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Bomang’ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro lengo ikiwa ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua papo hapo.

Sauti za wananchi wakiwasilisha kero zinazowakabili.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya mtaa wa Gezaulole na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali walioibua kero zinazowakabili ikiwemo mbwa kung’ata watu mtaani pamoja na baadhi ya wazee kukosa huduma za afya bure.

Wananchi wa kata ya Bomang’ombe wakiwa katika mkutano wa hadhara.(picha na Eliya Sabai)

Akitatua kero hizo Bomboko amezitaka mamlaka zilizopo wilaya ya Hai kuwa karibu na wananchi na kuwasaidia pindi wanapopata shida kwa kuchukua hatua za haraka  na pia amemtaka afisa mifugo wa kata ya Bomango’ombe kushirikiana nae kwa ukaribu  kuakikisha mbwa wanaowauma wananchi mtaani wanaua kwa kupigwa risasi na kwamba maafisa maendeleo ya jamii wanatakiwa kuhakikisha wazee wanapatiwa vitambulisho maalumu ambavyo watavitumia katika kupata matibabu bure.

Bomboko amesema watendaji wa serikali hawatapimwa kwa kukaa kwenye viyoyozi ofisini bali watapimwa kwa namna kero za wananchi zitakavyotatuliwa kwa wakati.

“sisi watumishi na watendaji wa serikali atutopimwa kwa kukaa ofisini kwenye viyoyozi, tutapimwa kwa huduma tunaziwahudumia wananchi na lazima tutoke tukawahudumie wananchi” Amesema Bomboko.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Hai Hassan Bomboko.

Mbali na kuwasilisha kero zao na kupata utatuzi  wananchi hao wamempongeza Bomboko kwa moyo wake wa kujitolea na kuwatumikia huku wakisifu utendaji wake wa kazi na kumuomba aendelee kuwa karibu yao ili awasaidie zaidi.

Mwananchi wa kata ya Bomang’ombe akiwasilisha kero yake(picha na Eliya Sabai)

Bomboko amekuwa na mikutano ya mara kwa mara ambayo ni endelevu ili kujua wananchi wa wilaya ya Hai wanakabiliwa na changamoto zipi ili zitatuliwe kwa wakati.

Sauti za wananchi wakimpongeza mkuu wa wilaya ya Hai.