Boma Hai FM

CCM yaibomoa CHADEMA Kingereka

20 May 2025, 10:10 am

Wanachama na Viongozi wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wakifurahi pamoja na mwenyekiti wa Kingereka aliyechaguliwa kwa tiketi ya Chadema baada ya kuhamia CCM (Picha na Henry keto)

Mapokezi ya mwenyekiti wa mtaa wa Kingereka aliyechaguliwa kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kuhama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Na Henry keto, Hai-Kilimanjaro

Mwenyekiti wa mtaa wa Kingereka A Dastan kimaro aliyechaguliwa kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA leo amerudisha kadi ya chama hicho na kuhamia chama cha Mapinduzi CCM

Dastani ameshukuru chama cha mapinduzi kwa kukubali ombi lake la kuhamia kwenye chama hicho jambo liliopokelewa kwa furaha kubwa na viongozi na wanachama wa chama hicho na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kwa maslahi ya wananchi wote, vilevile amewashukuru wananchi wa kingereka kuendelea kumuamini na kumchagua kuwa kiongozi wao

Sauti ya Mwenyekiti wa Kingereka A akIzungumza baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM akitokea CHADEMA

Mwenyekiti wa kata ya Bondeni exaudi Abinadabu Masawe amewaasa wenyeviti wote wa kata ya bondeni kujenga usawa kwa wananchi na safu ya uongozi kuanzia juu chini na kati ili wananchi waweze kuleta matatizo yao kwa viongozi wao.

Mwenyekiti wa Tawi la CCM kingereka Ndg Hashim swai pamoja na mwenyekiti wa kingereka A baada ya kuhamia CCM kutoka CHADEMA (Picha na Henry keto)
Mwenyekiti wa kata ya Bondeni Exaudi massawe akiongea na viongozi na wananchama wakati wakumpokea Dastani kimaro kutoka CHADEMA

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi tawi la kingereka ndg Hasheem sway amempongeza mwenyekiti Dastani na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika utendaji kazi akiwa ni mwananchama na mwenyekiti wa kingereka kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM tawi la kingereka Ndg Hashim Swai akimkaribisha Dastani kimaro akitokea CHADEMA