Boma Hai FM

Wahitimu VETA watakiwa kuleta mabadiliko kwa jamii

18 May 2025, 10:38 am

Mkuu wa wilaya ya Moshi Mkoani kilimanjaro Godfrey Mzanva akihutubia wakati wa mahafali ya 40 ya chuo cha VETA Mkoani Kilimanjaro (Picha na Furaha Hamad)

Mkuu wa wilaya ya Moshi Godfrey Mzanva ameshiriki mahafali ya 40 ya chuo cha VETA Moshi- Kilimanjaro ambapo wahitimu 155 wamehitimu na kuwataka kutumia maarifa na ujuzi kuleta maendeleo endelevu kwa jamii na kujiepusha na makundi mabaya ya kihalifu.

Na Henry keto, Moshi- Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Mkoani Kilimanjaro Godfrey Mnzava amewataka wahitimu wa chuo cha mafunzo ya Ufundi na Stadi ( VETA) kilichopo mkoani Kilimanjaro kujiepusha na makundi mabaya pindi warudipo nyumbani kwao

Amewataka kujihadhari na makundi mabaya yakiwemo ya Madawa ya kulevya,Mapenzi ya jinsia moja, na kuwataka kulinda Afya zao dhidi ya Magonjwa.

Mzanva amewasihi wahitimu hao kuwa ujuzi na maarifa ambayo wameyapata yalete mchango kwenye Taifa hili na sio vinginevyo na wanapaswa kujitambua wao ni nguvu kazi ya Taifa na ndio tegemeo la Taifa la leo na la kesho.

Mnzava ameyasema hayo Mei,16,2025 wakati akizungumza katika Mahafali ya 40 ya chuo hicho.

Amesema Taifa hili tangu misingi yake limesimamishwa na Vijana ambao walijitoa kwa moyo kwa Taifa lao, walisimama na kutumia maarifa yao ,jitihada na jasho lao kuhakikisha Taifa linafikia hatua hii ambayo imefikia.

Mnzava amesema wahitimu hao watarudi mtaani na watapokelewa na makundi mbalimbali huko mtaani ,na kuwataka kujihadhari na kamwe wasikubali kuingia kwenye makundi mabaya ambayo yataharibu maisha yao na wakiingia katika makundi hayo hasara yake itakuwa kubwa kwa maisha yao na kwa jamii inayowategemea pamoja na wazazi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godfey Mzanva akitoa hotuba wakati wa magafali ya 40 ya chuo cha VETA moshi-Kilimanjaro
Kaimu Mkurugenzi Veta kanda ya Kaskazini Ramuald Mlelwa akihotubia wakati wa mahafali ya 40 ya chuo cha VETA moshi (Picha na Furaha Hamadi)

Kaimu Mkurugenzi Veta Kanda ya Kaskazini Romuald Mlelwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza Vyuo vya VETA kwa kila Wilaya hasa kwa Mkoa wa Kilimanjaro,kila Wilaya tayari vyuo vimeanza kujengwa.

Baadhi ya wahitimu hao wakizungumza na vyombo vya Habari wameahidi kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliohaswa ,huku wazazi nao wakishukuru Uongozi wa chuo kwa kuwa na watoto wao kwa miaka yote mitatu kwa kuwafundisha,kuwalea kimwili, kiroho na kiakili.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi Veta Kanda ya Kaskazini Romuald Mlelwa wakati akitoa hotuba yake kwenye mahafali ya 40 ya chuo cha veta Moshi-kilimanjaro