Boma Hai FM
Boma Hai FM
16 May 2025, 12:50 pm

Crdb bank wilayani Hai mkoani Kilimanjaro yajenga darasa moja la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya Msingi Uswaa lenye thamani ya Shilingi Millioni 25 ,hafla ya makabidhiano yafanyika.
Na Henry keto .Hai-Kilimanjaro
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu amepokea darasa moja lenye thamani ya Shilingi Milioni 25 lililojengwa Kwa ufadhili wa Bank ya CRDB kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya Msingi Uswaa wilayani Hai.
Katika uzinduzi huo ametoa wito kwa Wananchi kulitunza darasa hilo ambalo ni muhimu sana hasa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, pia amewaomba Wananchi kuwa Karibu nao na kuwapa kipaumbele na upendo kama ilivyo kwa watoto wengine kwenye familia.
Aidha ameishukuru Bank ya CRDB kwa kujitolea kujenga darasa hilo na kuomba kuendelea kufanya hivyo kwasababu imekuwa ni desturi kwao kufanya hivyo, pia amewaomba Wananchi wa Kilimanjaro kujitoa kufanya maendeleo wasisuburi serikali ifanye, pale inapowezekana wao kufanya wafanye ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Vile vile ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa Fedha kwaajili yakuendeleza na kujenga miradi mingine mipya ambapo kwa kipindi cha miaka minne ameshatoa zaidi ya Trilioni 1.2 kwaajili ya kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe.Nurdin Babu ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuboresha taarifa zao katika daftari la kupiga kura kwa awamu ya pili linaloanza May 16,2025.
Amewatoa hofu Wananchi kuhusu zoezi la upigaji kura utakuwa wa amani na utulivu hakuna lolote baya litajitokeza, Serikali ya Mkoa kwakushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imejipanga vizuri kulinda amani wakati wote wa uchaguzi, hivyo Wananchi wajitokeze kupiga kura.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Bank ya CRDB ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa Wananchi wake,na bank inaunga mkono juhudi za kuleta maendeleo kwa Wananchi wote, vile vile ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya hai kwa kuusimamia mradi wakati wa ujenzi hadi kukamilika kwa viwango vinavyohitajika mpaka kufikia kukabidhi darasa kwaajili ya matumizi.
Katika hotuba yake amesema bank ya CRDB watakarabati Madarasa mawili ya shule hiyo kwaajili yakuunga mkono juhudi za Serikali na ikiwa ni miongoni mwa sera zao ambazo ni Afya, Elimu na Mazingira, na wanaendelea kutekeleza.