Boma Hai FM

Walioacha shule watakiwa kurudi kuendelea na masomo

8 April 2025, 11:27 am

Mkuu wa shule ya Sekondari Keni Renatus Lyimo( picha na Salma Sephu)

Katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Keni iliyopo wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wazazi na walezi wamekumbushwa kuwarejesha shule wanafunzi wote walioacha masomo kutokana na changamoto mbali mbali kwani ni haki yao kupata elimu.

Na Elizabeth Mafie

Serikali kupitia wizara ya elimu ya sayansi na teknolojia inatoa fursa kwa wanafunzi wote wenye umri kati ya miaka kumi na tatu hadi ishirini na moja (13-21)walio acha shule kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo mimba na utoro kurudi shule kusoma kwa njia m’badala na kufanya mtihani pasipo kulipia gharama yoyote.

Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Keni(picha na Salma Sephu)

Hayo yameelezwa na Patrick Leyana wakati  akimuwakilisha waziri wa elimu sayansi na teknolojia professa Adolf Mkenda ambaye pia ni mbunge wa  Rombo katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Keni.

Sauti ya mkurugenzi wa usajili wa shule Patrick Leyana wakati akimuwakilisha mbunge wa Rombo Profesa Adolf Mkenda.

Patrick Leyana ambaye ni mkurugenzi wa usajili wa shule amesema elimu bora kwa vijana itawasaidia kuendesha maisha yao kwa ufanisi zaidi.

Mwajuma Saguti ambaye ni kaimu afisa elimu sekondari akimuwakilisha mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya Rombo amesema kipo kituo wilayani hapo Kilamfua sekondari ambacho kinapokea wanafunzi waliocha shule kwa sababu mbali mbali .

Sauti ya Mwajuma Saguti kaimu afisa elimu sekondari wilaya ya Rombo.
Kaimu afisa elimu sekondari wilaya ya Rombo Mwajuma Saguti(picha na Salma Sephu)

Akizungumza mkuu wa shule ya sekondari Keni mwalimu Renatus Lyimo amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa uzio wa shule hali inayo sababisha utoro,wizi wa mali za shule na majirani kuingia eneo la shule bila utaratibu