TARI yawanoa wakulima, maafisa ugani Hai na Siha
11 September 2024, 11:43 am
Kutokana na zao la parachichi kuonekana zao lenye tija na la kibiashara Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) wameendesha mafunzo kwa maafisa kilimo pamoja na wakulima ili wajue namna bora ya kulima zao hilo.
Na Elizabeth Mafie.
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ( TARI) wameendesha mafunzo kwa maafisa ugani pamoja na wakulima zaidi ya arobaini kuhusu namna bora ya kulima zao la parachichi.
Mafunzo Hayo yamefanyika Septemba 10, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai yaliyo wahusisha maafisa ugani pamoja na wakulima kutoka wilaya ya Hai na Siha mkoani Kilimanjaro.
Mafunzo Hayo yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa wilaya Hai Lazaro Twange ambapo amesema kuwa anawashukuru wadau wote ambao wamebuni na kuwezesha mafunzo Hayo kufanyika Kwani Kwa sasa Kwa msaada Wadau Hao kilimo Ni biashara na kwamba serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri katika sekta hiyo.
” Mimi niwashukuru wote ambao mmebuni na mmewezesha shughuli hii kufanyika,sasa hivi Kwa msaada wa wadau kilimo ni biashara ,na serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwekeza katika sekta hii” amesema Lazaro
Aidha Lazaro amewasihi maafisa ugani hao pamoja na wakulima waliohudhuria mafunzo hayo wanatakiwa kujitendea haki wao wenyewe Kwa kujifunza Kwa weledi katika mafunzo hayo ili kuweza kujua zaidi kuhusu zao Hilo la parachichi na namna ya kuzuia vinyemelezi na maadui wanaohatarisha kilimo.
Kwa upande wake mkuu wa divisheni ya kilimo na uvuvi halmashari ya wilaya ya Hai David Lekei amesema kuwa zao la parachichi limeonekana kuwa zao la biashara na kwamba asilimia Sabini ya wananchi wa wilaya ya Hai na Siha wanajishulisha na kilimo hivyo watafiti wameona ni vyema wakulima pamoja na maafisa ugani kujifunza zaidi kuhusu zao la parachichi pamoja na kujua changamoto ya zao hilo na namna ya kukabiliana nazo na namna ya kufanya ili kupata parachichi bora linaloweza kuleta faida kubwa.
Naye Dkt. Abdullah Mkiga ambae Ni mtafiti kutoka Tari – Ukiriguru amesema kuwa waliona ni vyema kutoa mafunzo hayo kwa maafisa ugani pamoja na wakulima kutoka wilaya ya Hai na Siha Kwa lengo la kuwafundisha mbinu husishi za kudhibiti wadudu wahabaribifu wa matunda na kwamba kwa mkoa wa Kilimanjaro matunda yanayolimwa zaidi ni parachichi hivyo wamejikita zaidi katika zao hilo ili wale wakulima wanaolima wafahamu jinsi ya kitambua visumbufu na jinsi ya kuvithibiti na kuongeza kuwa kazi hiyo wanaifanya kwa kushirikiana na taasisi ya utafuti wa wadudu Icipe kutoka Nairobi na mradi huo unafadhiliwa na Giz.
Nao maafisa ugani na wakulima waliopatiwa mafunzo hayo wamewashukuru wadau hao kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani yatawasaidia katika kilimo cha parachichi na kulima kilimo chenye manufaa ili kuweza kujikwamua kiuchumi.