Boma Hai FM

Dc Mkalipa aongoza zoezi la upandaji miti eneo la utalii Chemka

23 May 2024, 10:57 am

Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa akipanda mti katika chemchem ya chemka ambapo ni eneo la utalii wa maji moto(picha na Elizabeth Mafie)
Kaimu mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Patris Otieno akipanda mti katika chemchem ya chemka ambapo ni eneo la utalii wa maji moto (picha na Elizabeth Mafie)
Wananchi wakipanda miti(picha na Elizabeth Mafie)

Katika kuendelea kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji,mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa ameongoza zoezi la upandaji miti katika chemchem ya chemka na chemchem ya Rashidi Kombo na kuwataka wananchi na wafanyabiashara wa maeneo hayo kuwa na utamaduni wa kupanda miti.

Na Elizabeth Mafie

Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa amewataka wananchi  wa kijiji cha chemka pamoja na  wafanyabiashara  wa eneo  la chemka  kata ya Masama Rundugai kuwa na utamaduni wa kupanda miti majumbani mwao pamoja na sehemu zao za biashara kwani jambo la kutunza mazingira ni la kila mmoja na kwamba bila mazingira eneo la utalii chemka haliwezi kuwepo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa.

Mkalipa ameyasema hayo wakati akiongoza zoezi la upandaji  miti katika chemchem ya chemka ambapo ni eneo la utalii wa maji moto pamoja na chemchem ya Rashidi Kombo zoezi liloloshirikisha  wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Mkalipa amesema kuwa wanapanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira na kwamba ni muendelezo wa maelekezo ya serikali kupitia ofisi ya makamu wa Rais wizara ya muungano na mazingira kwani kila wilaya ilitakiwa kupanda miti milioni moja laki tano kwa mwaka huu na kwa wilaya ya Hai wameshafikia lengo   hilo na wameendelea kupanda miti  maeneo mbalimbali hivyo ni vyema miti hiyo ikatunzwa ipasavyo.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Hai Amiri mkalipa akiwataka wananchi kutunza miti hiyo.

Kwa Upande wake Kaimu mkurugenzi wa Bonde la mto Pangani Patris Otieno  ambao ndio waratibu wa zoezi hilo la upandaji miti  kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Hai,Ofisi ya mkurugenzi pamoja na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) amesema kuwa katika kuendeleza kampeni ya utunzaji na upandaji wa miti kando kando ya mito, chemchem, na maeneo oevu  wamepanda jumla ya miti mia sita  na lengo ikiwa ni kuendelea kuihifadhi vyanzo vya maji katika maeneo ya Bonde  ikiwa  ni zoezi endelevu na kwamba  tayari wameshapanda miti ipatayo milioni moja na laki tano kwa wilaya ya Hai lakini lengo lao ni kuendelea kupanda miti elfu tatu katika kipindi hiki.

Amesema kuwa swala la uhifadhi wanafanya kwa kushirikiana na wadau  wa mazingira wakiwemo wananchi wanaozunguka  maeneo hayo,taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali na kwamba wanatoa elimu ili watu waweze kujua jinsi ya kuhifadhi maeneo ya vyanzo  na kuhakikisha kwamba hakuna shughuli zozote za kibinadamu zinazofanyika katika maeneo hayo.

Sauti ya kaimu mkurugenzi Bonde la Mto Pangani Patris Otieno.

Nae mtaalamu wa misitu kutoka ofisi ya maliasili halmashauri ya wilaya ya Hai John Katikiro  amesema kuwa wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kutunza na kufuatilia miti inayopandwa katika maeneo ya wilaya ya Hai na kwamba wamekuwa wakiwachukulia hatua wale wote wanaobainika kufanya uharibifu wa mazingira.

Sauti ya mtaalamu wa misitu halmashauri ya wilaya ya Hai John Katikiro.

Nao wananchi na wafanyabiasha katika chemchem ya Chemka wamesema kuwa wamefurahishwa na zoezi hilo la upandaji miti na kuhaidi kutunza miti hiyo kwani miti ni sehemu yao na kwamba kupitia miti hiyo wanapata fursa ya kufanya biashara kutokana na watalii kwenda kwa wingi katika chemchem hiyo.

Sauti ya Regina Zacharia mfanyabiasha katika eneo la utalii Chemka.