Profesa Mkenda akutana na warombo waishio Dar es salaam,wajadili maendeleo.
7 May 2024, 12:10 am
Wanananchi kutoka Rombo Mkoani Kilimanjaro waishio Dar es saalam wakutanishwa na Mbunge wao na kujadili kuhusu maendeleo ya Rombo na namna ya kutatua changamoto mbalimbali.
Na Elizabeth Mafie
Mbunge wa Rombo Profesa Adolf Mkenda ambae pia ni waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia hapa nchini amefanya mkutano na wananchi wa Rombo waishio Dar es Salaam lengo ikiwa ni kujadiliana Kwa pamoja kuhusiana na maendeleo yaliyofanyika Rombo na yanayoendelea kufanyika pamoja nakuzitolea ufafanuzi Kero watakazoziibua.
Mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Rombo wanaoishi Dar es Salaam,baadhi ya wabunge wa mkoa wa Kilimanjaro na madiwani kutoka Kata 28 za Halmashauri ya Rombo pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo umefanyika katika ukumbi wa Cadnal Adam uliopo Msimbazi Center jijini Dar es saalam.
Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa amekuwa na utararibu wa kuelezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika Rombo ikiwemo miradi ya barabara,Afya,maji,na Elimu na kwamba sio Mara ya kwanza kufanya hivyo bali ni muendelezo na atakuwa anafanya hivyo ili wananchi wote waelewe maendeleo ya Rombo.
“Utaratibu huu tumeanza sio Jana ,sio juzi Ni tangu zamani tulianza Arusha, Dodoma na Leo tuko Dar es Salaam, lengo Letu hapa Ni kueleza namna tunawajibika, tunafanya sana mikutano Rombo, juzi hapa tumefanya mkutano tarafa ya Mwengwe viongozi wote tumekutana, na tulikuwa na power point kuelezea nini kimefanyika Kila Kata na takatoka tukaenda kwenye mkutano wa hadhara Kingachi, Kwa hiyo hatuji hapa kanakwamba ni Mara ya kwanza,haya mambo tunayafanya kule”Amesema Mkenda.
Kwa upande wake mwananchi wa Rombo anayeishi Dar es Salaam Felisian Mtenga amesema kuwa wamefurahishwa na Jambo hilo la kukutana Kwa pamoja na kujadiliana kuhusu maendeleo ya Rombo na kwamba wangependelea kuanzishwa Kwa Benk ya Rombo kwani wanapokuwa na benki yao ni rahisi kufanikiwa lazima kuwa na benki ,pamoja na kupata mtaji wa kuanzisha viwanda na kuwa na uchumi endelevu.
Nae Mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mangwala amesema kuwa wilaya ya Rombo wameenda kutekeleza miradi mingi ya maendeleo,Kwa kupata fedha kutoka serekali kuu na kwamba wamepokea shillingi bilioni 12 Kwa ajili ya miondombinu pekee,hivyo Kazi inaendelea Rombo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amempongeza Mbunge wa Rombo Profesa Adolf Mkenda na kwamba wananchi wa Rombo wamepata Mbunge anaefanya Kazi nzuri hivyo wamuunge mkono ili aweze kuhitimisha Kazi hiyo.