Waliochukua mikopo Hai watakiwa kurejesha
23 February 2024, 10:06 am
Vikundi vya vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kurejesha mikopo waliyochukua katika halmashauri ya wilaya hiyo kama utaratibu unavyoelekeza.
Na Janeth Joachim
Wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kurejesha fedha za mikopo ya halmashauri zinazotolewa kwa vikundi mbalimbali vikiwemo vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa na Elia Kapinga kutoka ofisi ya mkurungezi wilaya ya Hai division ya maendeleo ya jamii alipozungumza katika kipindi Cha siku mpya kinachofanywa na Radio Boma Hai Fm nakuwataka baadhi ya vikundi kuacha tabia ya udanganyifu pindi wanapohitaji mikopo au wakati wa urejeshaji.
Aidha amesema vikundi au mtu binafsi ambao watashindwa kurejesha mikopo hiyo sheria zitachukuliwa dhidi yao kwa kufikisha kituo Cha polisi, mahakamani na wakati mwingine kuuziwa vitu vyao vyenye thamani.
Pia Kapinga amesema kuelekea siku ya mwanamke duniani kwa kauli mbiu isemayo “wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii” inamtaka mwanamke kuwezeshwa kiuchumi kwa kutoa mikopo kwa lengo la kuinua uchumi wa mwanamke kijamii na kitaifa kwa ujumla.
Naye Afande Asha kutoka kituo Cha polisi Boma Ng’ombe kitengo Cha dawati la jinsia na watoto amewataka wanawake kutambua nafasi zao katika jamii kuelekea kilele Cha maadhimisho ya siku mwanamke duniani.
Maadhimisho ya siku mwanamke hufanyika kila mwaka na katika wilaya ya Hai yatafanyika katika kata ya Machame Kijiji cha Narumu na kuanza tarehe 1 march hadi tarehe 8 March ikiwa ni kilele chake.