Pambazuko FM Radio
Matumizi ya teknolojia ya kilimo shadidi
28 December 2024, 7:12 pm
Na Katalina Liombechi
Wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji wameshauriwa kutumia teknolojia ya kilimo shadidi inayozingatia matumizi sahihi ya rasilimali maji ambayo haiathiri uendelevu wake.
Mkuu wa Idara ya Kilimo Halmashauri ya Mlimba Mhandisi Romanus Myeye ameyasema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Radio Pambazuko FM ambapo ameeleza kuwa mbali na teknolojia hiyo kuongeza tija pia inatumia eneo dogo, mbegu kidogo, palizi kidogo, mbolea kidogo kwa kushauriwa na wataalam, maji kidogo lakini wakati wote kipato ni kikubwa huku vyanzo vya maji vinakuwa endelevu na kwamba jamii nzima inanufaika.
KIPINDI KUHUSU KILIMO CHA UMWAGILIAJI