Pambazuko FM Radio
Mbolea, madawa katika zao la kokoa-Kipindi
27 December 2024, 2:29 pm
Na Katalina Liombechi
Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Dkt Yuda mgeni amewataka wakulima wa kokoa kutumia Mbolea za asili husaidia kuongeza idadi ya viumbe hai kwenye udongo, kama vile bakteria na fungi wanaosaidia kuvunja na kusambaza virutubisho kwenye mizizi ya mmea.
Amesema matumizi ya mbolea za asili katika kilimo cha kakao yana manufaa mengi, yakiwemo kuboresha ubora wa udongo, kupunguza gharama, na kulinda mazingira
Ameeleza kuwa hiyo ni njia endelevu na rafiki kwa mazingira ambayo inachangia katika uzalishaji wa kakao yenye tija.
KIPINDI KUHUSU MBOLEA NA MADAWA KATIKA ZAO LA KOKOA