Pambazuko FM Radio

Muda mzuri wa kupanda, kutunza shamba la kokoa-Kipindi

21 October 2024, 1:15 pm

Na Katalina Liombechi

Wakulima wa kokoa wanashauriwa kuzingatia kanuni bora za kilimo kwa kupanda na kufanya palizi kwa wakati ili kuvuna kwa tija.

Kwa mujibu wa Afisa Kilimo Kijiji cha Mbingu Sister Eusebia Punduka, kupanda kokoa kwa wakati ni muhimu hasa msimu wa mvua unapoanza kwani inahitaji mvua ya kutosha ili kuota na kukua vizuri.

Aidha katika kutunza zao hilo amesema inashauriwa kufanya palizi na jembe la mkono ili kutifulia mmea na kurahisisha kupata lishe.

Tunapanda kwa wakati kwa sababu mkulima lazima atumie kanuni bora za kilimo

KIPINDI KUHUSU KUPANDA NA KUTUNZA SHAMBA LA KOKOA(PALIZI)