Highlands FM
Highlands FM
10 July 2025, 12:41

Hakuna anayepanga kuugua au kuumia, lakini afya yako inaweza kubadilika kwa kufumba na kufumbua.
Na Samwel Mpogole
Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanajiunga na huduma za bima ya afya ili kuepuka changamoto za gharama kubwa za matibabu pale wanapopatwa na madhila ya kiafya.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mbeya, Eliud Kilimba, alipokuwa akizungumza na kituo hiki ofisini kwake, ambapo amesema kuwa bima ya afya ni suluhisho la kudumu kwa familia nyingi zinazokumbwa na changamoto za ghafla za kiafya.
Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya wameeleza kuwa bado kuna uhitaji wa elimu zaidi kuhusu namna ya kujiunga, faida zake, na namna bima hiyo inavyofanya kazi katika vituo vya kutolea huduma za afya.
NHIF imeendelea kushirikiana na serikali za mitaa na wadau wa afya katika kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya.
