Highlands FM
Highlands FM
10 July 2025, 12:48

Vitendo vya rushwa katika uchaguzi ni kati ya vikwazo vya kuwa na uchaguzi unaozingatia misingi ya haki na usawa kwa kuwa vinavyoathiri haki na fursa ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Na Samwel Mpogole
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya imesema kuwa kuelekea uchaguzi mkuu, imejielekeza zaidi katika kusimamia na kulinda maadili kwa kupambana na vitendo vyote vya rushwa, huku ikiendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mapambano hayo.
Akizungumza na kituo hiki, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Maghela Ndimbo, amesema mafanikio ya vita dhidi ya rushwa hayawezi kupatikana kwa nguvu ya taasisi hiyo pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa karibu na wananchi wa kada mbalimbali.
Aidha, Mkuu huyo wa TAKUKURU amewataka viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kukemea na kuelimisha waumini kuhusu madhara ya rushwa kwa jamii na maendeleo ya taifa.
