Boma Hai FM
Boma Hai FM
11 June 2025, 10:37 am

Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yamefanya mkutano wa pamoja katika kuweka mikakati yakufanya kazi kwa pamoja na kubainisha changamoto zao kwenye uongozi wa wilaya ya Hai
Na Henry Keto. Hai-Kilimanjaro
Mashirika yasiyo ya kiserikali yametakiwa kukaa pamoja kuweka mikakati yakufanya katika kuihudumia jamii.
Matakwa hayo yametolewa na Mratibu wa mashirika hayo wilaya ya Hai Ndg Elia Kapinga katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambapo mashirika 15 yameshiriki katika mkutano huo.
Kapinga ameyataka mashirika hayo NGO’s kukaa pamoja kuweka mikakati na kushirikiana katika utendaji kazi kwasababu yanaisaidia serikali kuhudumia watu, vile vile ameyaasa mashirika hayo Kuachana na tamaduni zisizofaa na zisizo za kiafrika na kitanzania.
Mohamed ally ni mwenyekiti wa kituo cha Sober house and helping hand foundation taasisi inayotoa elimu na kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya (Uraibu) ametoa wito kwa wote waliothirika au walevi kupondukia kufika kituoni kwao ili kupata msaada ili kujikomboa kutoka kwenye Uraibu.
Pia ameeleza sababu za Uraibu muda mwingine ni mtindo wa maisha, mapenzi, maumivu ya utotoni au malezi mabaya ya utotoni, mawazo ya maisha na nyingine kadhalika.

Fred vendeline ni kijana aliyeathirika na madawa ya kulevya kwa muda mrefu kuanzia mwaka 1990’s baada ya kuhangaika kwa muda mrefu akapatiwa matibabu kwenye kituo cha Kilimanjaro New vision Sober house iliyopo Bomang’ombe Hai Kilimanjaro na kupona kabisaaa mpaka Sasa ana miaka 9 bila matumizi ya madawa
Ameeleza aina za Uraibu sio madawa ya kulevya tu Bali hata POMBE za kawaida, matumizi ya Cm kupitiliza, mapenzi kupitiliza na ngono za jinsi moja,Kubet na aina nyingine nyingi za Uraibu.