Boma Hai FM
Boma Hai FM
27 May 2025, 8:47 pm

Askofu mstaafu wa kwanza wa TAG Dkt Immanuel Lazaro aliyefariki mei 17 2025 azikwa kijijini kwao Mudio wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Na Elizabeth Mafie. Hai-Kilimanjaro
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amesema kuwa Tanzania imeondokewa na Kiongozi Bora wa dini aliye hakikisha ustawi wa Imani na ukomavu wa watu Kiroho unakuwa vizuri.
Ametoa kauli hiyo Mei 27,2025 Katika Kijiji Cha Mudio Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za pole kwa familia,waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God -TAG na waombolezaji wengine kutoka ndani na nje ya Nchi walio hudhuria mazishi ya aliye kuwa Askofu Mstaafu wa Kwanza wa TAG Dkt.Immanuel Lazaro aliyefariki Mei 17,2025 akiwa na umri wa miaka 88.
“Sisi watu wa Imani lazima tukuwe na tukomae,kukomaa ni pamoja namna wewe kutokusomewa mstari kwenye Biblia unaenda kula nyasi pale nje ,kukomaa ni pamoja na wewe kutokusikia habari fulani na wewe unakimbilia huko una enda kunywa mambo ya ajabu ajabu,tukuwe na tuongezeka kwa Imani” Dkt.Tulia
Amesema kuwa watu wanapo omba kupewa muda mrefu wa kuishi na Mungu wanapaswa kuwa na sababu za kuomba kuishi maisha marefu ili wafanye kazi kama alizokuwa kifanya Hayati Askofu Dkt.Lazaro enzi za uhai wake kwa kutoa huduma za Kiroho na kijamii

Aidha amewataka viongozi wa dini na waumini kuendelea kuombea Taifa hasa wakizidisha maombi katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu.