Boma Hai FM
Boma Hai FM
22 April 2025, 11:46 am

Mkuu wa wilaya ya Rombo Raymond Mwangwala akizungumza na waandishi wa habari.
Kutokana na wilaya ya Rombo kuwa na migogoro mingi itokanayo na ardhi kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid imetajwa kutatua changamoto hiyo.
Na Elizabeth Mafie
Kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia Legal Aid wakaazi wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro wapo mbioni kuondokana na changamoto ya Migogoro ya Ardhi ambayo imekuwa ikiwakabili kwa Kipindi kirefu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mh.Raymond Mwangwala wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Rombo.
Amesema Rombo imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa ardhi kutokana na asili ya mazingira ya Rombo ambapo maeneo mengi hurithiwa kwa koo na familia .
Ameeleza Kuwa kesi nyingi katika viamba ambavyo hurithiwa zinatokana na wanafamilia kuuza maeneo pasipo ushirikishwaji wa wanafamilia wengine
Hata hivyo amemshukuru Mh.Rais kwa kuja na kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid kwani imesaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua migogoro ya ardhi.