

31 March 2025, 1:44 pm
Ikiwa ni sikukuu ya Eid-el-Fitir kote duniani, ambapo waumini wa dini hiyo mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Hai watakiwa kuendelea kuishi maisha ya kumpendeza mwenyenzi Mungu na kuendelea kulinda amani.
Na Elizabeth Mafie
Waumini wa Dini ya kiislamu mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuendelea kudumisha amani katika kuelekea uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.
Hayo yamesemwa Machi 31 2025 na Sheikh wa mkoani Shaabani Mlewa wakati wa Maadhimisho ya sikukuu ya Eid-el-Fitir iliyofanyika Msikiti wa Shafii Bomango’mbe wilayani Hai mkoani hapa.
Akizungumza na waumini hao mara baada ya swala hiyo ya Eid ,amewataka Waislamu kuendelea kudumisha amani na upendo kwani ndiyo msingi mzuri wa maisha.
“Ni kweli uchanguzi mkuu unakuja,na kila uchanguzi unapokuja uinakuja na vitimbwi vingi , sasa akili kichwani,wewe mwenyewe kama muislamu inatakiwa kuwa wa kwanza kutunza amani”amesema Mlewa
Aidha katika uchanguzi ujao amewataka Wananchi kuchagua viongozi wazuri , ambao watawaongoza na wanaoamini lakini pia waumini hao wajitokeze na kugombea nafasi mbalimbali.
“nyinyi wenyewe ingieni Tupate watu tutakao waamini,watakao tusaidia ,tunaitaji maendeleao,ukienda Kwa Mwenyekiti wa kijijii kusiwe na ukirutumba ,nataka kumuonea Mbunge anakata simu hapana,tunataka Viongozi wazuri wasema ukweli”. Amesema Shekhe Mlewa.
Awali Imamu wa Msikiti huo, Athumani Hamis,amesema kuwa anamshukuru Mungu kwakuhitimisha vyema mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwamba waumini wa dini hiyo wanapaswa kuyaishi yale waliyoelekezwa katika kipindi chote cha mfungo.
Hivyo kuwakumbusha waumini kuendelee kufanya mema kama walivyokuwa wakifanya wakati wa mfungo wa Ramadhan,kwani kurudi kufanya maovu ni jambo baya mbele ya Mwenyezi Mungu na unahesabika kuwa umepata hasara.