

26 March 2025, 12:55 pm
Kutokana na uvumi kuhusu shule ya msingi Nkwenshoo kuwa ina waalimu watatu pekee na wote wameomba uhamisho,radio Boma Hai Fm imefika ili kukuletea ukweli wa jambo hilo.
Na Eliya Sabai
Kufuatia taarifa potofu inayosambaa mitandaoni ya kwamba shule ya msingi Nkwenshoo iliyopo katika kata ya Machame Mashariki wilayani Hai inawalimu watatu pekee na wote wameandika barua ya kuhama shuleni hapo huku ukabila ukiusishwa kama chanzo cha tatizo ilo.
Radio Boma Hai fm imefunga safari mpaka shuleni hapo ilikuweza kupata taarifa kiundani kuhusu jambo hilo na hapo ndipo ilifanikiwa kuzungungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo huku akitanabaisha wazi kupokea taarifa hizo kwa masikitiko kwani hazina ukweli wowote na huku akinadi kuwa wao wanafanyakazi ili kuhakikisha wanainua taaluma shuleni hapo.
Mwandishi wetu alifanikiwa kuzungumza na Rumisha Shoo ambaye ni mzazi wa mwanafunzi aliyepo shuleni hapo nae alikemea vikali jambo hilo huku akisema walimu na wazazi katika shule hiyo wamekuwa na mahusiano mazuri yasiyotiliwa shaka.
Diwani wa kata hiyo James Mushi pamoja na diwani wa viti maalum ambao ndio viongozi wa kata hiyo wameelezea kusikitishwa na taarifa hiyo ambayo imeleta sintofahamu kwani wakazi wa eneo hilo wanaishi vizuri na walimu wa shule hiyo na kwamba hakuna changamoto yeyote kati yao kama wanavyoelezea.
kwa upande wake diwani wa viti maalum Hausen Nkya amempongeza mchungaji wa kanisa la usharika wa Nkweshoo (KKKT) lililopo karibu na shule hiyo kwa kukemea vikali upotoshaji wenye lengo la kuchafua taswira ya Hai
Kupitia uchunguzi wetu na kujiridhisha pasipo shaka tumegundua shule hiyo yenye wanafunzi 168 ina jumla ya walimu 7 ambao watano ni ajira rasmi huku wawili wakiwa ni wa mafunzo kwa vitendo na hakuna mgogoro wowote na huku wanafunzi na walimu wakiendelea na majukumu yao kama kawaida