Hai yang’ara wiki ya maziwa
30 May 2024, 11:18 am
Wilaya ya Hai yaadhimisha wiki ya maziwa,katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro awapongeza kwa uwaandaji.
Na Riziki Lesuya
Katibu tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Tixon Nzunda ametoa pongezi kwa uongozi wa wilaya ya Hai kwa kuandaa maadhimisho ya wiki ya maziwa yanayo adhimishwa tarehe 28/05/2024 hadi tarehe 1/06/2024.
Nzunda ametoa pongezi hizo wakati akifungua maadhio hayo kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega yanayofanyika katika viwanja vya snow View wilayani Hai, ambapo amesisitiza umuhimu wa wananchi kunywa maziwa.
“Mhe. Waziri na katibu Mkuu wameniambia niwapongeze kwa kujitoa, kujipanga na kuthamini siku hii ya maziwa duniani ambapo kitaifa inafanyika kule Mwanza, na kwa sababu hiyo wameniagiza kwamba mwaka 2025 Mungu akituweka hai Wizara itaandaa kwa kushirikiana na ninyi Hai.
Lakini la pili nimeomba mitamba ya ngombe wa maziwa ili Hai nayo ipate mitamba bora kwa ajili ya kuzalisha maziwa, ni matumaini yangu kwamba wizara haitatutupa.” Ameeleza
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa amemuomba katibu Tawala kufikisha maombi ya wilaya ya kupata mbegu bora kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa maziwa wilayani Hai.
tunakuomba Katibu Tawala wa mkoa utufikishie maombi yetu kwa waziri ,wilaya ya Hai inazalisha maziwa mengi kwa mkoa wa Kilimanjaro tuonaomba , atupatie mbegu mpya za kisasa za uzalishaji wa maziwa kwasababu hayo ndio mambo yetu tuliyo yazoea, maziwa haya tunayo kusanya tunayakusanya kwa ubora ili tuweze kutengeneza soko
Awali akisoma taarifa ya maziwa Mkuu wa Divisheni Kilimo, Mifugo na Uvuvi David Lekei amesema katika wilaya ya Hai maziwa yanasindikwa na vyama vya ushirika vya maziwa alivyo vitaja kuwa ni Nronga, Kalali, Marukeni, Nguni, Mamba pamoja na vyama vingine.
Naye Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka ameahidi halmashauri kuendelea kuwawezesha wazalishaji na wafugaji wa ngombe wa maziwa kwa kuwawekea mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na mikopo isiyo na riba inayo tokana na mapato ya ndani mara baada ya dirisha kufunguliwa.