SHIUMA Hai kufanya maonesho mwenge wa uhuru 2024
7 March 2024, 5:22 pm
Hai Kuelekea kuashwa kwa mwenge kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 2 April wafanyabiashara wadogowadogo maarufu machinga wilayan Hai wameaanda maonyesho makubwa ya bidhaa mbalimbali za utamaduni sanaa na utalii
Na Janeth Joachim
Kuelekea kuashwa kwa mwenge kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 2 April wafanyabiashara wadogowadogo maarufu machinga wilayan Hai wameaanda maonyesho makubwa ya bidhaa mbalimbali za utamaduni sanaa na utalii yatakayofanyika katika viwanja vya shule ya Hai day kuanzia April 1 hadi April 4 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na katibu wa shirikisho la wamachinga wilaya ya Hai (SHIUMA) Paul Mwalongo alipozungumza na waandishi wa habari pamoja na wamachinga katika ukumbi wa Dolfin na kusema lengo la maonyesho hayo ni kutumia fursa waliyopata kutoka serikalini ya mwenge kuwashwa katika mkoa wa Kilimanjaro na kupita katika ukaguzi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mwalongo amesema kufika kwa mwenge katika wilaya ya Hai kutazindua mradi wa SHIUMA wa wilaya ya Hai.
Naye katibu wa SHIUMA mkoa wa Kilimanjaro Stevin Kavishe amewataka wananchi na wamachinga kujitokeza kwa wingi katika kuupokea na kuulaki mwenge wa uhuru 2024.
Kwa upande wa machinga wameleza kuwa wamejipanga kwa kuonyesha bidhaa mbalimbali.
Maonyesho hayo ya SHIUMA yana kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru isemayo “Tunza Mazingira na shiriki katika uchaguzi wa serikali za mtaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu”.