Waharibifu vyanzo vya maji kukiona
29 January 2024, 1:04 pm
Bodi ya maji Bonde la Pangani kwa kushirikiana na Jumuiya ya watumia maji mto Kware wamewataka wananchi katika kata ya Masama Magharibi wanaoharibu vyanzo vya maji kwa kukata miti kuacha mara moja na badala yake watunze vyanzo hivyo.
Na Elizabeth Mafie
Serikali za vijiji na vitongoji zimetakiwa kutoa ushirikiano kwa jumuiya za watumia maji ili kotokomeza uharibifu wa mazingira unaofanywa katika maeneo ya hifadhi na vyanzo vya maji na kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa.
Wito huo umetolewa na Brown Mwangoka ambaye ni mtaalam wa mazingira kutoka bodi ya maji Bonde la Pangani wakati wa ukamati wa mtuhumiwa wa ukataji miti katika chemchem ya Mlilie wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Ameeleza kuwa wao kama bodi ya maji Bonde la Pangani wanapongeza serikali za vijiji na vitongoji zinazo fanya vizuri katika uhifadhi wa mazingira na kwamba wanawataka viongiozi wa vijiji watoe ushirikiano kwa jumuiya ili kuzuia shughuli zote za kuharibu vyanzo vya maji ambavyo vinategemewa katika mustakabili wa maisha ya binadamu.
Mwangoka amesema wanaunga mkono jitihada hizo kwa kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa kwa mujibu wa sheria, kwani ukifanya shughuli za uharibifu wa vyanzo vya maji ndani ya eneo la hifadhi sheria ya usimamizi wa mazingira no 20 ya mwaka 2014 kifungu no 57 pamoja na sheria ya rasilimali maji zinakataza kufanya sshughuli kwenye maeneo hayo.
Amesema kwa mujibu wa sheria faini ya kosa hilo ni kuanzia mili1 hadi 10 kulingana na aina ya uharibifu uliofanywa hivyo mtuhumiwa huyu atafunguliwa mashutaka kwa mujib wa sheria na kuhakikisha kwamba anapatiwa adhabu anayostahiki ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Amesema bonde la Pangani wanasimamia jumuia za watumia maji ambazo zimeundwa na wananchi kwa lengo la kufanya kazi kwa karibu ya uhifadhi wa mazingira.
Naye Wilifred Massawe Mwenyekiti wa juimuiya ya watumia maji mto kware amesema chanzo hicho kimeaharibiwa kumekatwa miti zaidi ya kumi na moja mtuhumiwa huyo alianza kutaka miti mwaka jana aliitwa polisi mara tatu lakini hakuitikia wito.
Ameeleza kuwa kwa mwaka huu mtuhumiwa huyo amekata miti sita ndipo wakaamua kushirikiana uongozi wa kijiji na wakampa taarifa kuwa asiendelea kukata mbao na magogo yasimame hadi shauri lake lisikilizwe ofisi ya kijiji lakini alikaidi agizo hilo na ndipo walipomkamata na kumpeleka katika vyombo vya sheria.
Amesema pamoja na kuwa wanapata ushirikiano kutoka serikali ya kijji changamoto waliyo nayo ni uharibifu wa mazingira na kwamba kazi inakuwa ngumu kutokana uhalifu kuwa ndani ya maeneo ya vijiji.
Kwa upande wake Mashoya Natai ambae ni diwani kata ya Masama Magharibi amesema wananchi wameitikia wito wa kutunza mazingira kwa kuotesha miti lakini kuna waharibifu wa chache ambao wanaharibu mazingira kwa kukata miti bila taratibu.