Wagonjwa hospitali ya Kibon’goto waridhika na huduma
23 January 2024, 12:59 pm
Wagonjwa mbalimbali kutoka hospitali maalum ya taifa ya magonjwa ambukizi kibon’goto waridhishwa na huduma.
Na Elizabeth Mafie
Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali maalumu ya Taifa ya magonjwa ambukizi Kibong’oto iliyopo wilayani Siha mkoani Kilimnjaro Dkt Leornad Subi amesema hospitali hiyo itaendelea kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri bila kulalamika .
Dkt Subi ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika hospitali hiyo katika hafla ya uzinduzi wa mawili yaliyolewa na Serikali aina ya Land cruces yenye thamani ya shilingi milioni 400.
Kwa mujibu wa Dkt Subi,hospitali hiyo iliita watu kutoka nje kufanya utafiti kuona wagonjwa katika hospitali hiyo wanaridhika na huduma inayotolewa katika hospitali hiyo ya Taifa ya magonjwa ambukizi
Dkt Subi amesema asilimia 97% ya Wagonjwa wanaopatiwa huduma kutika katika hospitali hiyo maalumu wanaridhika na huduma zinazotolewa na wataalamu katika hospitali hiyo. Hospitali ya Taifa ya magonjwa ambukizi Kibong’oto ni hospitali ya Taifa na inatumia sayansi zaidi katika uchunguzi na ufuatiliaji wa wagonjwa ndio maana zaidi ya aslimia 75 ya wagonjwa wanaotibiwa hapo wanapona na wanarudishwa nyumbani ndio kwamaana huduma ni nzuri zaidi.