Wananchi Hai watakiwa kutunza mazingira
18 January 2024, 12:16 pm
Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa awataka wananchi kutunza mazingira.
Na Elizabeth Mafie
Wananchi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kulinda na kutunza mazingira ili kuhifadhi vyanzo vya maji dhidi ya uharibifu na kubaki salama kwaajili ya vizazi vijavyo.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa katika zoezi la kupanda miti katika chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Nguni kata ya Masama Kati,ambapo amesema kuwa watakao bainika wamefanya uharibu wa chanzo cha maji kwa namna yoyote ile hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na atawajibika kulipa faini nakupanda miti katika eneo hilo.
Aidha wakala wa huduma za misitu TFS wilaya ya Hai Marisia Alois ameeleza kuwa wamejipanga vyema katika kudhibiti uharibifu wa mazingira hususani ukatakaji miti ovyo na kulima kwenye vyanzo vya maji kwani wanavyombo imara vya kudhibiti uharibifu huo.
Kwa upande wake afisa mazingira kutoka bodi ya maji bonde la Pangani Brown Mwangoka akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Bonde la Pangani amesema kuwa wameweka mabango matatu kwenye mipaka ya vyanzo vya maji yakuonyesha katazo la kufanya shughuli za kibinadamu katika chanzo cha maji ikiwa ni pamoja na kupanda miti zaidi ya mia tano katika chanzo hicho
Kwa mujibu wa , Brown ameishukuru serikali ,taasisi na wadau mbalimbali kwa kuendelea kutoa ushirikiano wao katika jitiada zakuhakikisha ulinzi na utunzaji wa vyanzo vya maji unazingatiwa katika kupambana na changamoto wanazokumbana nazo kama kilimo, na ujenzi katika vyanzo vya maji.