Jamii yatakiwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji
13 December 2023, 10:30 pm
Diwani awaandalia tafrija fupi watoto wenye uhitaji.
Na Latifa Boto
Diwani wa kata ya Masama Magharibi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Mashoya Natai ameitaka jamii kuwasaidia watoto wenye mahitaji mbalimbali hususani katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ili waweze kusheherekea sikukuu hizo pamoja na kufanya maandalizi ya shule kwa mwaka 2024.
Ameyasema hayo leo hii katika tafrija iliyoandaliwa na wafadhili wa kituo cha Lukani Children center kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuwasaidia watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo nguo,vyakula kwa ajili ya kushehekea sikukuu ya christmass na mwaka mpya.
Amesema kuwa anawashukuru wafadhili hao ambao wamejitolea kwa kufanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha watoto hao wenye mahitaji kuwa ni sehemu ya jamii kama walivyo wengine kwa kuwapatia mavazi, vyakula pamoja na kuwachingia michango katika elimu mbayo ndiyo nyenzo muhimu kwa maisha yao.
Aidha Mashoya amesema kuwa kituo hicho cha lukani chidren center kina jumla ya watoto 59 ambao 32 wameshapatiwa ufadhili na 18 bado hawajapata ufadhili mbapo anaendelea kutafuta wafadhili ili watoto hao waliosalia wapate mahitaji ya msingi pamoja na elimu kwa kuwa wanatoka katika familia zisizojiweza.
Kwa upande wake Lightness Mushi ambaye ni mmoja wa wazazi wenye watoto katika kituo hicho cha lukanI chidren center amesema kuwa kituo hicho kimekuwa msaada kwao na kwamba wao kama wazazi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao pamoja na kuwaonyesha upendo pamoja na kuwafatilia kwa karibu kwani kwa nyakati hizi vitendo vya ukatili vimekidhiri katika jamii na pia baadhi ya wazazi wamejikita zaidi katika utafutaji .