Semina ya wajasiriamali
20 November 2021, 9:08 am
Madiwani wasaidieni wananchi kuzitambua fursa za kiuchumi: Diwani kata ya Bomang’ombe
Na Salma Shaban
HAI
Diwani wa kata ya Bomang’ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Evod Njau amewaomba madiwani kote nchini kuwasaidia wananchi wakimemo wajasiriamali ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi walizozitoa za kuwatumikia ipasavyo kwa kuwasaidia kuzitambua fursa mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Njau ametoa rai hiyo Nov 18 2021 katika semina ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo na wa kati, iliyoandaliwa na wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na diwani huyo na kufanyika katika ukumbi wa Bamboo uliopo Bomang’ombe.
CAST….DIWANI EVOD
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo Fatuma Msemo mkazi wa Bomang’ombe na Ismail Mushi wamemshukuru Diwani Njau kwa kuona umuhimu wa kuandaa semina hiyo kuwapatia elimu kwani wafanyabiashara wengi wanaojiunga kwenye vikundi wanapopata mkopo wanashindwa kurejesha kwa ufanisi kutokana na kukosa elimu ya urejeshwaji wa mikopo hiyo.
CAST….WASHIRIKI
Kwa upande wake mwezeshaji katika semina hiyo ambaye pia ni meneja wa NMB tawi la Hai Bw. Abraham Mbise ameeleza kuwa wafanyabiashara wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kukosa elimu ya matumizi ya fedha za mikopo hali ambayo imepelekea wao kama wadau wa maendeleo kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wajasiriamali.
CAST…MENEJA NMB
Jumla ya wajasiriamali 245 na vikundi 51 vya ujasiriamali katika kata ya Bomang’ombe vimeshiriki katika semina hiyo ya siku 3 lengo likiwa ni kujengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo pamoja na kuzitambua fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye kata hiyo.