Pambazuko FM Radio

Vijana Ifakara wanatakiwa kupambana kwa kufanya kazi na wasikate tamaa.

3 April 2024, 1:37 pm

Na Elias Maganga

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero amewataka vijana kupambana kwa kufanya kazi ili kuzikamilisha ndoto zao.

Mh, Lijualikali ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Pambazukofm kupitia Kipindi cha jioni leo,ambapo amesema Vijana wana wajibu wa kupambana kutengeneza maisha yao kadri wanavyoweza.

Akitolea mfano yeye mwenyewe wakati akiwa diwani,Mbunge na mpaka kuwa mkuu wa Wilaya amevumilia mengi makubwa na mazito lakini hakukata tamaa.

Amesema chochote unachoamua kukifanya tambua kuwa kina maumivu yake na gharama ya kulipa, hivyo unapaswa kuvumilia hiyo gharama utakayoilipa.

Dc Lijualikali amenukuu maandiko matakatifu yasemayo hapa dunia tunapita na maisha ya mwanadamu ni mafupi  na yamejaa taabu, lakini ukifanikiwa utaishi vizuri

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali akifanya mahojiano na Pambazukofm{Picha na Elias Maganga}
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali