Pambazuko FM Radio

DC Kilombero aagiza halmashauri kuharakisha mikopo ya vikundi

8 January 2025, 1:33 am

Picha ya hundi pesa zilizotolewa na halmashauri ya Mlimba kwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu – Picha na Isidory Mtunda

Na: Isidory Mtunda

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero mkoani wa Morogoro, Wakili Danstan Kyobya, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba kuhakikisha mikopo ya awamu ya pili inatolewa ndani ya mwezi Januari 2025 kwa vikundi vilivyobaki.

Vijana wakiwa kwenye pikipiki walizopata kwa mkopo – Picha na; Isidory Mtunda

Maagizo hayo yalitolewa Januari 6, 2025, wakati wa uzinduzi wa mikopo ya asilimia kumi kutoka mapato ya ndani. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Halmashauri ya Mlimba, zilizopo Itongoa, Kata ya Mngeta, Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro ambapo zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetengwa kwa ajili ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kilombero – D. Kyobya

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlimba, Mheshimiwa Innocent Mwagasa, alimhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa hawatatoza adhabu kwa kata ambayo ina vikundi visivyokamilisha marejesho. Badala yake, juhudi zitaelekezwa kushughulikia vikundi husika ili kuhakikisha uwajibikaji bila kuathiri maeneo mengine.

Sauti ya Mwangasa:

Katibu wa Kikundi cha Wanawake Kinara, Bi. Fadhila Idd Muro, pamoja na Mwenyekiti Mwajuma Yusufu kutoka Kata ya Mbingu, waliwataka wanawake waliopokea mikopo hiyo kuzingatia maadili ya familia. na walisisitiza umuhimu wa kurejesha mikopo kwa wakati ili kutoa nafasi kwa wengine kunufaika kupata mkopo.

Picha ya Fadhila Murro – Na; Isidory Mtunda

Sauti ya Fadhila na Mwajuma wa kikundi cha Wanawake Kinara